Jeremiah 9:17-20

17 aHivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,
waite wale walio na ustadi kuliko wote.

18 bNao waje upesi
na kutuombolezea,
mpaka macho yetu yafurike machozi
na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.

19 cSauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:
‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!
Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!
Ni lazima tuihame nchi yetu
kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”


20 dBasi, enyi wanawake, sikieni neno la Bwana;
fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.
Wafundisheni binti zenu kuomboleza;
fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.
Copyright information for SwhKC